Mark 14:14-19

14 aMwambieni mwenye nyumba ile atakayoingia, ‘Mwalimu anauliza: Kiko wapi chumba changu cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka?’ 15 bAtawaonyesha chumba kikubwa ghorofani, kilichopambwa tena kilicho tayari. Tuandalieni humo.”

16 cWale wanafunzi wakaondoka na kwenda mjini, nao wakakuta kila kitu kama Isa alivyowaambia. Hivyo wakaiandaa Pasaka.

17 dIlipofika jioni, Isa akaja pamoja na wale wanafunzi wake kumi na wawili. 18 eWalipoketi mezani wakila, Isa akawaambia, “Amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti, mmoja anayekula pamoja nami.”

19Wakaanza kuhuzunika na kumuuliza mmoja baada ya mwingine, “Je, ni mimi Bwana?”

Copyright information for SwhKC